Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Operesheni za misaada zinaingia hatua mpya Niger:WP

Operesheni za misaada zinaingia hatua mpya Niger:WP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanza operesheni kubwa ya kuwalisha watoto 67,000 na familia zao nchini Niger. Duru hii ni sehemu ya operesheni za shirika hilo kutaka kuwafikia watu takribani milioni nane walio na matatizo ya chakula katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi.

Kwa mujibu wa WFP watoto 67,000 walio na umri wa chini ya miaka miwili watapata mgao wa chakula kila mwezi chakula ambacho ni mchanganyiko wa mahindi na soya ili kukabiliana na utapiamlo. Wakati huo huo watu milioni 4 wa familia zao watapewa kilo 50 za mahindi au mchele, kilo tano za sukari na chumvi na mgao wa mafuta ya kupikia.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa WFP mjini Niamey Thomas Yanga watu wa Niger wameathirika sana na ukame na hivyo ni muhimu sana kupata msaada huo wa chakula.