Ban aelezea huzuni yake kufuatia vifo vya moto nchini Urusi

10 Agosti 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameelezea huzuni yake kufuatia vifo vilivyosababishwa na moto wa msituni uliolikumba eneo la nje ya Moscow nchini Urusi.

Duru za habari zinasema idadi kubwa ya watu wamekufa kutokana na moto huo unaochochewa na kiwango cha juu cha joto katika baadhi ya maeneo ya Urusi kutokana na hali ya ukame inayoendelea. Katika taarifa yake iliyosomwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa Ban ametoa salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na waliojeruhiwa na janga hilo.

Pia ameongeza kuwa anatambu juhudi kubwa zinazogfanywa na serikali ya Urusi kuudhibiti moto huo , na amehakikisha jukumu la Umoja wa Mataifa kwamba uko tayari kusaidia kwa njia yoyote ile endapo utaombwa kufanya hivyo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter