Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNPOS ndani ya Somalia itasaidia mchakato wa amani:Mahiga

UNPOS ndani ya Somalia itasaidia mchakato wa amani:Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amesema ana imani kwamba kuongezeka kwa uwepo wa ofisi yake ndani ya Somalia kutasaidia kupiga hatua ya mchakato wa amani.

Amesema katika miezi michache ijayo ofisi ya masuala ya siasa ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somalia UNPOS itaongeza idadi ya wafanyakazi wake wa kiamataifa na kitaifa mjini Garowe Puntland na Harigeisa Somaliland ili kuungana na wafanyakazi wa ofisi hiyo ambao tayari wako katika maeneo hayo.

Ameongeza kuwa baada ya hatua hiyo UNIPOS itahitaji kuwepo Moghadishu ingawa kwa sababu za kiusalama itabidi kuchukua tahadhari kubwa. Amesema kuna kazi kubwa ya kufanya kwa ushirikiano na serikali ya mpito ya Somalia, AMISOM, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadu wengine, pamoja na kukusanya taarifa , uongozi na majukumu ambayo ynawezekana tuu kama UNIPOS itakuwa ndani ya Somalia.

Kwa sasa kuna jumla ya wafanyakazi 60 wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa ndani ya Somalia na wengine karibu 800 wa kitaifa na kutoka mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wakiendesha shughuli za kutoa misaada.