Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko Pakistan ni moja ya janga kubwa la kibinadamu katika muongo uliopita:UM

Mafuriko Pakistan ni moja ya janga kubwa la kibinadamu katika muongo uliopita:UM

Mafuriko yaliyoikumba Pakistan yanaonekana kuwa ni moja ya janga kubwa kabisa la kibinadamu kuwahi kutokea katika muongo uliopita.

Serikali ya nchi hiyo inakadiria watu milioni 14 wataathirika kwa njia moja au nyingine huku mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa hivi sasa yakijitahidi kupeleka misaada ya dharura ya kibinadamu kwa watu milioni sita. Hata hivyo mashirika hayo yanakabiliwa na changamoto nyingi na bado hayajawafikia watu wote.

Watu wengi wameathirika kuliko hata waliokumbwa na tetemeko Haiti au walioathirika na tetemeko la 2005 nchini Pakistan. Andrej Mahecic kutoka shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema mashirika hayo bado yanahangaika kuwafikia waathirika.

(CLIP MAHECIC)

Mafuriko hayo pia yameathiri ghala la chakula la Umoja wa Mataifa na mahema na vifaa vingine vya kulalia. Barabara ambazo zimefurika na madaraja yaliyosombwa na maji pia vinaathiri ugawaji wa misaada kwa baadhi ya maeneo ambayo hadi sasa hayajafikiwa.