Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu imetoa msaada wa vitabu vya sheria kwa chuo kikuu nchi Kosovo

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu imetoa msaada wa vitabu vya sheria kwa chuo kikuu nchi Kosovo

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu inayoshughulikia kesi za uhalifu mbaya kabisa wa vita uliotendeka wakati wa vita vya Balkan miaka ya 1990, inasaidia ufadhili wa kisheria kwa kutoa msaada wa vitabu na majarida ya sheria kwa chukuo kikuu cha Kosovo.

Mahakama hiyo kwa ajili ya Yugoslavia ya zamani ICTY ambayo iko mjini The Hague Uholanzi ilitangaza mwishoni mwa wiki kwamba inatoa msaada wa majarida kwa kitivo cha sheria na kitengo cha haki za binadamu cha chuo kikuu cha Pristina.

Msaada huo umetolewa baada ya mkutano baina ya ofisi ya mahakama hiyo na maafisa wa chuo kikuu cha Pristina. Katika taarifa yake mahakama hiyo ICTY imesema imejidhatiti kuchagiza uheshimuji wa utawala wa sheria na inatumai kwamba vitavu hivyo vitawasaidia wanafunzi wa sheria nchini Kosovo.

Lengo la mahakama hiyo iliyoanzishwa baada ya azimio la baraza la usalama mwaka 1993 ni kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na mauaji ya , uhalifu, ubakaji wa wanawake na kuendelea na mauaji ya kikabila katika Yugoslavia ya zamani.