Wanyarwanda walioko Sudan wamepiga kura katika ubalozi wao mjini Khartoum
Wanyarwanda walioko Sudan leo wamepata fursa ya kushiriki upigaji kura wa uchaguzi mkuu wa Rais kupitia ubalozi wao ulioko mjini Khartoum.
Miongoni mwa watu hao ni wanajeshi wa kulinda amani wa vikosi vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID akiwemo kama wa vikosi hivyo Luteni jenerali Patrick Nyamvumba aliyesafiri kutoka Nyala Sudan Kusini hadi Khartoum kutekeleza haki yake ya kupiga kura.
Kituo maalumu cha upigaji kura kwenye ubalozi wa Rwanda Khartoum kimewekwa kwa ajili ya siku moja tuu ili kuwaruhusu raia wa Rwanda wengi wakiwa wafanyakazi wa UNAMID, UNMIS na mashirika mengine ya misaada kumchagua kiongozi wa nchi yao.
Vikosi vya Rwanda ni vya pili kwa ukumbwa katika mpango wa UNAMID baada ya Nigeria , vikiwa na askali na polisi zaidi ya 3,300 wa kulinda amani Darfur.