Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umelaani mauaji ya wafanyakazi wa afya nchini Afghanistan

UM umelaani mauaji ya wafanyakazi wa afya nchini Afghanistan

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan amelaani mauji ya wafanyakazi 10 wa afya Agosti 5 mjini Bahakhshan nchini Afghanstan.

Mwakilishi huyo Staffan de Mistura ameyaelezea mauaji hayo ambayo kundi la Taliban limekiri kuhusika kuwa ni kuso la jinai na ukatili mkubwa.

Amesema watu hao walikuwa Afghanistan ili kufanya kazi ya kuwasaidia masikini na watu waliokuwa katika hatari. Amesisitiza kwamba wafanyakazi wa afya lazima wapate fursa ya kuwatibu wanaohitaji huduma hiyo, na ni lazima wafanye hivyo bila hofu .

Ameongeza kwamba chini ya sheria za kimataifa wafanyakazi wa afya lazima walindwe wakati wakitimiza wajibu wao wa kuokoa maisha. Amesema wote waliohusiaka na mauaji hayo na matukio mengine yanayowalenga wafanyakazi wa afya lazima waheshimu thamani ya maisha ya watu. Amesema wafanyakazi wote wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan wameshtushwa na kusikitishwa na mauaji hayo.