Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM ajadili suala la mvutano kwenye kambi ya Kalma Darfur

Afisa wa UM ajadili suala la mvutano kwenye kambi ya Kalma Darfur

Mkuu wa vikosi vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika vya kulinda amani Darfur UNAMID amekuwa na mazungumzo na waziri wa Sudan kuhusu hali ya mvutano na hofu katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kalma.

Mkuu huyo Ibrahimu Gambari na waziri wa masuala ya jamii wa Sudan Mutrif Siddiq wamezungumzia mvutano na matukio yaliyojitokeza hivi karibuni kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kalma Kusini mwa Darfur na hali ya kambi ya Hamadiya.

Gambari amemuhakikishia waziri Siddiq nia ya UNAMID kushirikiana na serikali ya Sudan katika mazingira yaliyopo ya changamoto kwa ajili ya haki na maslahi ya watu wa Darfur. Pia amesema UNAMID imesikitishwa na matukio hayo ya karibuni na kufafanua kuhusu athari yanayoweza kusababisha katika mutakabali wa mchakato wa amani.

Na kuhusu suala la watu sita ambao wamepata hifadhi kwenye kituo cha UNAMID Gambari amesema sula hilo ni nyeti lakini unyeti wake usijekuleta kutoelewa na kuharibu ushirikiano mzuri uliopo baina ya serikali ya Sudan na UNAMID. Pia amemweleza waziri Siddiq kuhusu mkutano na serikali ya Sudan hapo Agost 5 na kuafikiana kuunda tume ya kushughulikia masuala ya Kalma na kuyapatia ufumbuzi.