Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wa Rwanda leo wamepiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais

Raia wa Rwanda leo wamepiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais

Raia takribani milioni tano wa Rwanda leo wamejitokeza kushiriki upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa Rais.

Wagombea wanne akiwemo Rais wa sasa Paul Kagame ndio wanaochuana katika uchaguzi huu wa pili baada ya mauaji ya kimbari nchini humo mwaka 1994.

Duri zinasema Rais Kagame na chama chake cha RPF wanapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo baada ya wapinzani wakubwa kushindwa kushiriki katika kinyang'anyiro cha uchaguzo huu. Kutoka Kigali mwandishi wetu Ramadhan Kibuga ambaye anafuatilia uchaguzi huo ametuandalia ripoti hii.

(RIPOTI KIBUGA)