Wiki ya kimataifa ya unyonyeshaji inatia nganga Agosti 7

6 Agosti 2010

Wiki ya kimataifa ya unyonyeshaji inamalizika Jumamosi Agost 7 na akauli mbiu mwaka huu ilikuwa ni kuainisha jukumu la wataalamu wa afya kuhusu suala hili.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF unyonyeshaji ni moja ya njia bora kabisa za kumlinda mtoto kiafya, hii ikimaanisha kwamba kumpa mtoto maziwa ya mama pekee bila chakula kingine chochote katika miezi sita ya mwanzo ya maisha yake. Wataalamu wa afya wanasema maziwa ya mama ni rahisi kulainika tumboni mwa mtoto na yana virutubisho vyote muhimu vya kumkuza na kumlinda dhidi ya magonjwa kwa kuhamisha kinga ya mama kwenda kwa mtoto kupitia maziwa.

Unyonyeshaji unatofautiana katika nchi mbalimbali na kutokana na sababu balimbali. Eneo la pembe ya Afrika kama Somalia imebainika kuwa wanawake hunyonyesha watoto siku chache sana hadi tatu tuu baada ya kuzaliwa. Huku nchi nyingine kama Chad hali ya hewa na migogoro imeonekana kuchangia kina mama wengine kuanza kuwalisha watoto vyakula vingine kabla ya kutimiza umri wa miezi sita.

WHO na UNICEF wamekuwa na mikakati maalumu ya kuhakikisha wataalamu wa afya wanawasaidia hususan kina mama wanaojifungua kwa mara ya kwanza kuelewa umuhimu wa kunyonyesha, jinsi ya kunyonyesha na kuelimisha juu ya athari za kutowanyonyesha watoto katika miezi sita ya mwanzo.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter