Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake Senegal wazalisha chumvi yenye iodine kunusuru na goita:WFP

Wanawake Senegal wazalisha chumvi yenye iodine kunusuru na goita:WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema upungufu wa madini ya iodine ni tatizo kubwa nchi Senegal linalosababisha athari kwa watoto wengi ugonjwa wa goita kwa watu wazima.

Wanawake wanaozalisha chumvi nchini humo wameamua kuwa msitari wa mbele kupambana na matatizo hayo kwa msaada wa WFP, ambao unasaidia kuongeza iodine kwenye chumvi wanayozalisha na kuwapa mafunzo.

Senegal ni moja ya wazalishaji wakubwa wa chumvi Afrika Magharibi na WFP imekuwa ikinunua asilimia 100 ya mahitaji ya chumvi ya watu wa nchi hiyo na pia mahitaji ya nchi jirani katika ukanda huo. Mradi huo wa WFp umeshavisaidia vijiji 28 na wazalishaji 700 ambao wanazalisha tani 500 za chumvi iliyoongezwa iodine kwa mwezi.