Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria, utulivu na uhalifu ndio changamoto zinazoikabili Liberia:UNMIL

Sheria, utulivu na uhalifu ndio changamoto zinazoikabili Liberia:UNMIL

Kamanda wa jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini Liberia UNMIL amesema changamoto kubwa zinazoikabili nchi hiyo hivi sasa ni masuala ya sheria, utulivu na kukabiliana na uhalifu.

Akiliarifu baraza la usalama hii leo kamanda huyo Luteni jeneral Sikander Afzal amesema changmoto hizo zinahusiana na matatizo ya usalama wa ndani. Amesema chanzo cha tatizo ni watu kutokuwa na imani na jeshi la polisi na mfumo wa sheria. Ameongeza nah ii ni kutokana na polisi kushindwa kuchukua hatua ipasavyo dhidi ya wahalifu, ingawa hali kwa sasa inaanza kubadilika.

Amesema lakini wakati huohuo mfumo wa sheria wa Liberia hauana uwezo wa kukabiliana ongezeko la kesi, na UNIMIL inahitaji kuingilia kati kusaidia. Kuhusu UNIMIL kamanda huyo amesema imepunguza uwezo wake wa kijeshi kutoka zaidi ya watu 14000 iliyokuwa nao hadi kufikia walinda amani 8000 na hii inamaanisha kwamba waliopo wanaongeza majukumu na hivyo inakuwa vigumu kupita katika wilaya zote na pia kuchukua hatua za haraka.