Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM alia na uhalifu wa ubakaji katika wakati wa migogoro

Afisa wa UM alia na uhalifu wa ubakaji katika wakati wa migogoro

Afisa wa Umoja wa Mataifa leo amesema ubakaji ni moja ya changamoto kubwa za amani na usalama duniani.

Na ameongeza kuwa ubakaji katika vita unasalia kuwa ni uhalifu ambao haulaaniwi kwa kiasai kikubwa na kuwafanya wahalifu wengi kukwepa mkono wa sheria. Afisa huyo Margo Wallstrom ambaye ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya ukatili wa kimapenzi katika vita amewaambia waandishi wa habari mjini New york kwamba ubakaji sio uhalifu wa dunia kuufumbia macho na kuuchukulia kama ni mila na makosa ya asili kama ambavyo yamekuwa yakiitwa mara nyingi.

Ameongeza kuwa katika vita hivi ubakaji sio athari bali ni vita vipya, kwani ni kosa dhidi ya mtendewa na pia ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.