Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala ya Mashariki ya Kati limetawala mazunguzo ya Ban na Bi Clinton

Suala ya Mashariki ya Kati limetawala mazunguzo ya Ban na Bi Clinton

Suala la mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati na juhudi za kurejelea mazungumzo kati ya Israel na Palestina ndio ilikuwa ajenda ya mazungumzo ya leo kati ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton.

Bwana Ban ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini Japan amezungumza na Bi Clinton mapema leo kwa njia ya simu kuhusu hali ya mashariki ya kati. Miongoni mwa mambo waliyoyachambua viongozi hao wawili ni jukumu la wanadiplomasia wa pande nne Quartet, wanaojumuisha Marekani, Muungano wa Ulaya, Urusi na Umoja wa Mataifa, katika kusaidia kuchagiza mchakato wa amani .

Wanadiplomasia hao wane wanaunga mkono mpango wa amani ya mashariki ya kati ulioidhinishwa kimataifa wa kuwa na suluhu ya mataifa mawili.