Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hongera Kenya kwa kupiga kura ya maoni kwa amani na utulivu:UM

Hongera Kenya kwa kupiga kura ya maoni kwa amani na utulivu:UM

Umoja wa Mataifa umekaribisha kura hiyo kwa kufanyika kwa amani na utulivu. Pia umewapongeza watu wa Kenya kwa kujitokeza kwa wiki kuamua ni jinsi gani wanataka kuongozwa siku zijazo nchini humo.

Afisa na mratibu wa masuala ya kikibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya Aeneas Chuma amesema katika mpya ni muhumu sana kwa Kenya hasa baada ya machafuko ya mwaka 2007 na kuidhinisha kwa kura ya maoni kumefungua ukurasa mpya katika historia ya Kenya baada ya kuipigania kwa miongo miwili.

Bwana Chuma ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa umekuwa msitari wa mbele wakati wote kuwachagiza Wakenya kudumisha amani na kutrumia haki yao ya kidemokrasia kupiga kura.

Na amesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana kwa karibu na serikali ya Kenya, jumuiya za kijamii na wadau wa maendeleo kuhakikisha kwamba ndoto za katiba mpya Kenya zinatimia. Mwandishi wetu Jason Nyakundi akiwa Nairobi ameshuhudia mchakato mzima wa kura ya maoni na kutuandalia makala hii.