Tanzania kuanza sensa ya watu wenye ulemavu hivi karibuni:UNDP

Tanzania kuanza sensa ya watu wenye ulemavu hivi karibuni:UNDP

Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limesema Tanzania itafanya sensa ya watu wenye ulemavu hivi karibuni.

Serikali ya nchi hiyo imeonyesha kwamba takwimu zilizopo za watu wenye ulemavu hazitoshelezi jambo ambalo linaathiri utoaji wa huduma kwa watu hao. UNDP inasema sensa hiyo itakuwa hatua moja mbele katika kujibu madai kwamba watoto wenye ulemavu ni lazima wawe sehemu ya mafanikio ya uandikishaji wa watoto wa shule za msingi katika nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki.

Mjada huo ulijitokeza katika warsha ya hivi karibuni iliyoandaliwa na UNDP, kitengo cha utafiti wa kuondoa umasikini na chuo kikuu cha Dar es salaam.