Chanjo dhidi ya polio imeanza nchi nzima Angola kwa msaada wa UNICEF
Kampeni ya siku tatu ya chanjo ya polio imeanza leo nchini Angola ikiwalenga watoto milioni 4.5 walio chini ya umri wa miaka mitano.
Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Marko Jimenez shirika hilo linaratibu kampeni kwa ushirikiano na shirika la afya duniani WHO na wizara ya afya ya Angola.
(SAUTI YA MARKO JIMENEZI )
Kwa mujibu wa UNICEF visa vya polio vimearifiwa katika majimbo sita ya Angola na visa 11 kutoka jimbo la Lunda kaskazini pekee. Shirika hilo limeonya kwamba polio ambayo imeanzia Angola sasa imesambaa hadi katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.