Skip to main content

Mashirika ya UM yanaendelea kwa kuwasaidia waathirika wa mafuriko Pakistan

Mashirika ya UM yanaendelea kwa kuwasaidia waathirika wa mafuriko Pakistan

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea na juhudi za kuwasaidia mamilioni ya waathirika wa mafuriko nchini Pakistan.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeonya kuwa nchi hiyo itakabiliwa na mafuriko zaidi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Shirika hilo limepanga kuwasaidia watu 350,000 na limeomba dola milioni 21 ili kukidhi mahitaji ya waathirika. Kati ya waathirika milioni nne watoto ni milioni 1.8 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, ambalo hadi sasa limeshawasaidia yatima 300 na kuwahamisha 52.

Ingawa sio waathirika wote wameshapokea msaada lakini shirika la mpngo wa chakula duniani WFP linasema limepeleka chakula cha mwezi mmoja kwa watu 237,000. Na limeongeza kuwa watu milioni 2.5 watahitaji msaada wa chakula katika miezi mitatu ijayo.