Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kidiplomasia za UM asia zahitaji uungwaji wa mkono:UM

Juhudi za kidiplomasia za UM asia zahitaji uungwaji wa mkono:UM

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limepongeza kazi za ofisi ya Umoja wa Mataifa inayosaidia nchi za Asia ya Kati kutatua matatizo mbalimbali, na kusisitiza kuwa kuna haja ya kuisaidia ofisi hiyo.

Ofisi hiyo ambayo ni kituo cha Umoja wa Mataifa cha masuala ya kidiplomasia Asia ya Kati UNRCCA kilianzishwa mwaka 2007 kuzisaidia serikali tano za eneo hilo kuongeza uwezo wake wa kuzuia migogoro kwa amani, kuchagiza majadiliano na kukabiliana na vitisho na changamoto za mipakani kama ugaidi, usafirishaji wa mihadarati, na uharibifu wa mazingira.

Kituo hicho kilichopo Ashgabat, Turkmenstan kinaongozwa na Miroslav Jenca ambaye ni mwakilishi wa Katibu ambaye leo ameliarifu baraza la usalama kuhusu miezi sita ya kazi yake. Katika taarifa ya baraza hilo iliyosomwa na Rais wa mwezi huu ambaye ni balozi wa Urusi Vitaly Churkin Baraza limepongeza kazi ya ofisi yake katika eneo hilo la Asia ya Kati na hasa hali ya hivi karibuni nchini Kyrgystan.