Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Masuala ya haki za binadamu ni muhimu sana kwa amani Nepal:UM

Masuala ya haki za binadamu ni muhimu sana kwa amani Nepal:UM

Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Nepal OHCHR-Nepal Richard Bennet leo amesema kushulikia masuala ya haki za binadamu ni muhimu sana nchini Nepal.

Amesema pia kuwachukulia hatua wanaokiuka haki hizo kutasaidia katika mchakato wa amani, katika nchi hiyo inayojaribu kujijenga upya baada ya muongo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Bwana Bennett na waziri mkuu wa Nepal Madhay Kumal wakiwa mjini Khathmandu, wamejadili uhusiano uliopo kati ya hali ya haki za binadamu na mchakato wa amani.

Afisa huyo ambaye atahitimisha jukumu lake hivi karibuni nchini humo mara kadhaa amewatolea wito serikali na wafuasi wa Kimao kutekeleza mkataba wa amani waliotia sahihi 2006 na kumaliza miaka kumi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyokatili malisha ya watu takribani 13,000.