Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati likiongeza muda wa mpango wa UM Iraq baraza la usalama limesisitiza serikali itakayojumuisha wote

Wakati likiongeza muda wa mpango wa UM Iraq baraza la usalama limesisitiza serikali itakayojumuisha wote

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limeongeza muda wa mpango wake nchini Iraq UNAMI kwa mwaka mmoja zaidi.

Baraza hilo pia limetoa wito kwa viongozi wa serikali kuongeza juhudi za kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itajumuisha pande zote. UNAMI inawajibika kuisaidia serikali ya Iraq katika masuala ya uchaguzi, maridhiano, kutatua migogoro ya mipaka, masuala ya haki za binadamu na mambo mengine ya kibinadamu yanayotia mashaka, ujenzi mpya na maendeleo.

Bila kupingwa baraza hilo limepitisha azimio namba 1936 ambalo limeamua UNAMI itaendelea kusalia Iraq hadi tarehe 31 Julai mwaka 2011 kama ilivyopendekezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ripoti yake ya karibuni kuhusu UNAMI. Wajumbe 15 wa baraza hilo pia wamesisitiza kwamba changamoto za usalama bado zipo nchini Iraq na kwamba marekebisho yanahitajika kwa njia ya majadiliano na umoja wa kitaifa.