Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakenya wako mbioni kupata katiba mpya baada ya kuiidhinisha kwa kura ya maoni

Wakenya wako mbioni kupata katiba mpya baada ya kuiidhinisha kwa kura ya maoni

Wananchi wa Kenya wameunga mkono kwa kiasi kikubwa kupata katiba mpya baada ya kusema ndio kwenye kura ya maoni iliyofanyika jana.

Kwa mujibu wa matokeo Katiba hiyo mpya, inaonekana kupingwa vikali katika mkoa wa Rift Valley ambao uliathirika sana ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Katiba hiyo,pia inatarajiwa kuzuia hali ya machafuko kama hayo yasitokee tena, ikiwa ni pamoja na kushughulikia maswala muhimu kama ya ardhi.

Rais Mwai Kibaki na waziri Mkuu Raila Odinga walikuwa vinara wa kampeni ya ndio katika katiba hiyo huku waziri wa elimu ya juu William Ruto akiongoza kampeni ya hapana. Mwandishi wetu Jason Nyakundi ameandaa taarifa hii kutoka Nairobi.