Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iraq inahitaji juhudi zaidi kufikia malengo ya maendeleo ya milenia:UM

Iraq inahitaji juhudi zaidi kufikia malengo ya maendeleo ya milenia:UM

Ripoti mya iitwayo malengo ya maendeleo ya milenia nchini Iraq inasema Iraq inahitaji kuongeza juhudi zaidi ili kufikia malengo hayo, yaliyoafikiwa na viongozi wa dunia mwaka 2000 ya kuimarisha hali ya maisha ya watu ifikapo 2015.

Ripoti hiyo iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa na serikali ya Iraq inasema hata hivyo nchi hiyo imepiga hatua katika baadhi ya maeneo kama njaa, vifo vya watoto wachanga na usawa wa kijinsia. Lakini imeainisha kwamba kuna hatua ndogo sana katika suala la kuandikisha watoto wa shule za msingi, kukabiliana na tatizo la ajira, kupata maji safi na salama ya kunywa na huduma za usafi.

Serikali ya Iraq na Umoja wa Mataifa wamekubaliana kuongeza juhudi kushughulikia masuala hayo ifikapo 2015, na hususani kupunguza pengo lililopo kati ya vijijini na mijini.