Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia bila silaha za nyukilia kuwaenzi vyema waliokufa Nagasaki:Ban

Dunia bila silaha za nyukilia kuwaenzi vyema waliokufa Nagasaki:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameungana na maelfu ya watu wa Nagasaki Japan kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya waliouawa mwaka 1945 kwa shambulio la bomu la atomic.

Amewaambia waombolezaji kwamba amefika Japan ili kutoa heshma zake na kuhudhuria kumbukumbu ya tukio ambalo halitosahaulika duniani, na kuungana na wale wanaosema daima tukio hilo halitotokea tena.

Watu zaidi ya 75,000 waliouawa Nagasaki na idadi kama hiyo Hiroshima baada ya Marekani kudondosha mambomu ya nyuklia mwezi Agosti mwaka 1945. Ban amesema watu wa Nagasaki na Hiroshima wamekuwa chachu kubwa katika juhudi za kimataifa za upokonyaji wa silaha za nyuklia

(SAUTI YA BAN KI-MOON-NAGASAKI)

Ban amesema na hilo ni swala analolipa kipaumbele, kwa ajili ya watu wa Japa, watu wa Korea, na watu wote wa dunia nzima. Naye Annika Thunborg msemaji wa CTBTO aliyerejea kutoka Hiroshima amesema ukijionea yaliyowasibu watu wa Nagasaki na Hiroshima utatambua ubaya wa silaha za nyuklia.

(SAUTI YA ANNIKA -HIROSHIMA)

Kesho Ijumaa Katibu Mkuu ataungana na mamilooni ya Wajapani katika kumbukumbu ya miaka 65 ya shambulio la bomu la atomic mjini Hiroshima.