Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya milioni 4 wameathirika na mafuriko nchini Pakistan:OCHA

Watu zaidi ya milioni 4 wameathirika na mafuriko nchini Pakistan:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema zaidi ya watu milioni 4 wameathirika na mafuriko ya Pakistan ambayo ymeshakatili maisha ya watu zaidi ya 1600.

Mratibu wa OCHA nchini humo Manuel Bessler amesema watu wamejikuta wakichanganyikiwa na pia kuwa na hasira hasa wakitambua kwamba msimu wa mvua za monsoon ndio kwanda uko katikati na hali inaonekana itakuwa mbaya zaidi kabla ya kupata afueni. Ameongeza kuwa idadi ya waathirika wa mafuriko hayo mabaya kuwahi kutokea kwa miaka 80 itaongezeka.

(SAUTI MANUEL BESSLER )

Mashirika ya misaada yanasema ingwa juhudi za kuwafikishia msaada walengwa hadhiridhishi lakini baadhi wamepokea msaada. Zaidi ya watu 200,000 wamepokea chakula, 700,000 wamepata maji safi ya kunywa huku maelfu ya mahema pia yameshagawiwa.