Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakenya wamemaliza kupiga kura ya maoni ya katiba kwa amani na utulivu

Wakenya wamemaliza kupiga kura ya maoni ya katiba kwa amani na utulivu

Wananchi wa Kenya leo wamepiga kura ya maoni ya katiba mya kwa amani na utulivu. Kura hiyo iliyoelezwa kuwa ni muhimu sana imeshuhudia idadi kubwa ya watu waliojitokeza kushiriki.

Vituo vya upigaji kura vimefungwa saa kumi na moja jioni saa za Afrika ya Mashariki na wale waliokuwa kwenye misururu tuu hadi wakati huo ndio walioruhisiwa kupiga kura.Rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga wote wamekuwa msitari wa mbele kuwachagiza wananchi kushiriki kura ya leo.

Katiba hiyo mpya inayopendekezwa, inatazamiwa kubadilisha mwelekeo wa siasa za Kenya, na kuwaepusha raia wa nchi hiyo kujikuta katika tafrani kama iliyoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu wa Desemba mwaka 2007. Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi meshuhudia upigaji kura huo na hii hpa taarifa yake.