Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iraq imefikia wakati nyeti baada ya uchaguzi wa bunge:Ad Melkert

Iraq imefikia wakati nyeti baada ya uchaguzi wa bunge:Ad Melkert

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Ad Melkert amesema Iraq imefikia mahali nyeti sana kufuatia kumaliza kwa mafanikio uchaguzi wa bunge Machi 7 na kuidhinisha matokeo ya uchaguzi huo Juni pili.

Melkert ameyasema hayo leo kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa wakati likifikiria kuongeza muda wa mpango wa msaada wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI. Bwana Melkert amesema licha ya miezi kadhaa ya majadiliano shughuli ya kuahamishia mamlaka kwa serikali mpya bado haijafanyika.

Pia ameelezea hofu yake kwamba kuendelea kuchelewa kuunda serikali mpya kunachangia sintofahamu ya Iraq na kuweka mazingira ambayo yanaweza kutumiwa na watu wanaopinga mabadiliko ya kidemokrasia nchini humo.

Amesema [ia kumekuwepo na dalili za kutia moyo kwani makundi makubwa ya kisiasa yanaonekana kuafikiana kuhusu haja ya kuwa na serikali ya umoja na wamekuwa wakijadili mipango ya kugawana madaraka.