Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano na naibu waziri Mohamed Aboud kuhusu kura ya maoni kwa amani Zanzibar

Mahojiano na naibu waziri Mohamed Aboud kuhusu kura ya maoni kwa amani Zanzibar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza watu wa Jamhuri ya Tanzania na haswa visiwa vya Zanzibar kwa kupiga kura ya maoni hivi karibuni kwa amani na utulivu.

Amesema ametiwa moyo na jitihada za watu wa Zanzibar za kuwa na hatma ya amani na mshikamano na kusema Umoja wa Mataifa uko tayari kuwasaidia kufikisha lengo hilo.

Flora Nducha wa Redio ya Umoja wa Mataifa amezungumza na naibu waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki wa kutoka Tanzania, Mohamed Aboud.