Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu awapongeza Watanzania kwa kupiga kura ya maoni kwa amani Zanzibar

Katibu Mkuu awapongeza Watanzania kwa kupiga kura ya maoni kwa amani Zanzibar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza watu wa Jamhuri ya Tanzania na haswa visiwa vya Zanzibar kwa kupiga kura ya maoni hivi karibuni kwa amani na utulivu.

Ban amekaribisha makubaliano baina ya vyama viwili vikubwa vya kisiasa nchini humo, Chama cha Mapinduzi CCM na Civic United Front CUF ambayo yalichagiza kura hiyo ya maoni lenye lengo la kufungua njia ya muafaka wa muda mrefu.

Katibu Mkuu amesema ametiwa moyo na jitihada za watu wa Zanzibar za kuwa na hatma ya amani na mshikamano na kusema Umoja wa Mataifa uko tayari kuwasaidia kufikisha lengo hilo