Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Haki za Binadamu kuchunguza tuko la flotilla Gaza

Baraza la Haki za Binadamu kuchunguza tuko la flotilla Gaza

Baraza la haki za binadamu nalo linachunguza tukio la flotilla lilitokea Gaza Mai 31 ili kubaini nini hasa kilichosababisha shambulio hilo.

Hata hivyo kwa mujibu wa Rais wa baraza la haki za binadamu Sihasak Phuangketkeow uchunguzi wa baraza hilo utakuwa unalenga kitu kidogo tofauti na uchunguzi uliotangazwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mapema wiki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva amesema tume ya uchunguzi ya watu watatu itajikita tuu katika kuangalia ukiukwaji wa sheria za kimataifa katika masuala ya kibinadamu na haki za binadamu .

Ameongeza kuwa kila tume ya uchunguzi itakuwa na jukumu lake na ya baraza la haki za binadamu inachotafuta kujua ni uhalali wa kisheria wa tukio la Mai 31 ambapo makomandoo wa Israel walishambulia msururu wa meli za misaada na kusababisha vifo vya Waturuki tisa. Rais wa baraza amesema ni muhimu baraza kuchunguza kesi za madai ya kukiuka haki za binadamu

(SAUTI YA SIHASAK)

Ameongeza kuwa uchunguzi uliotangazwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa utakuwa unaangalia masuala mbalimbali na hususani njia za kuzuia kutokea tena kwa tukio la flotilla. Israel imeafiki ushirikiano na uchunguzi huo lakini imekataa kutoa ushirikiano kwa tume ya uchunguzi ya baraza la haki za binadamu.