Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF inaendelea kuwasaidia mamilioni ya waathirika wa mafuriko Pakistan

UNICEF inaendelea kuwasaidia mamilioni ya waathirika wa mafuriko Pakistan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaendelea kupleka misaada ya kuokoa maisha kwa mamilioni ya waathirika wa mafuriko nchini Pakistan wengi wao wakiwa watoto na wanawake.

Mafuriko hayo ynayosemekana kuwa mabaya zaidi kuwahi kutokea kwa miaka 80 yameathiri watu milioni 3.2 wakiwemo watoto milioni 1.4, ambao wote wanahitaji msaada wa dharura. UNICEF imekuwa ikitoa msaada wa vifaa vya usafi, madumu ya maji na biskuti kwa watoto na familia.

Pia imekuwa ikikarabati visima 73 vinavyowanufaisha watu 800,000. Imeomba dola milioni 10.3 kwa wahisani wa kimataifa ili kukidhi mahitaji ya waathirika hao.