Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amewataka vijana Japan kuwa viongozi wa kupinga silaha za nyuklia

Ban amewataka vijana Japan kuwa viongozi wa kupinga silaha za nyuklia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anayeendelea na ziara nchini Japan leo amezungumza na wanafunzi wa chuo kikuu.

Katika chuo kikuu cha Waseda amewaasa wanafunzi hao kuwa viongozi wa upokonyaji wa silha ili kumbukumbu ya Hiroshima na Nagasaki isisahaulike. Ban amewaambia vijana hao kwamba ili ndoto ya kuwa na dunia huru bila silaha za nyuklia iweze kutimia basi vijana wote duniani lazima wawe na lengo moja.

(CLIP BAN JAPAN)

Ban amesema Umoja wa Mataifa unahitaji ubunifu, nguvu na upeo wa vijana wa Japan. Pia amekutana na waziri mkuu wa nchi hiyo Naoto Kan na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo sialha za nyuklia. Kesho Ban atakuwa mjini Nagasaki kabla ya kuhudhuria kumbukumbu ya Hiroshima siku ya Ijumaa.