Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa zamani wa Rwanda ahukumiwa miaka 25 kwa mauaji ya kimbari

Afisa wa zamani wa Rwanda ahukumiwa miaka 25 kwa mauaji ya kimbari

Afisa wa zamani wa serikali ya Rwanda amehukumiwa kwenda jela miaka 25 kwa kushiriki katika mauaji ya mwaka 1994 yaliyokatili maisha ya Watutsi wengi na Wahutu wa mzimamo wa wastani nchini Rwanda.

Dominique Ntawukulilyayo aliyekuwa kiranja wa Gisara jimbo la Butare amekutwa na hatia ya kola la mauaji ya kimbari. Mahakama imebaini kwamba kati ya tarehe 20 na 23 Aprili mwaka 1994 maelfu ya Watutsi na familia zao walikimbia mashambuliko kwenye miji yao na kupata hifadhi kwenye soko la Gisara.

Wengi wa Watutsi hao waliondoka sokoni na kwenda katika mlima wa Kibuye baada ya Ntawukulilyayo kuwaahidi kwamba watakuwa salama na kupata chakula huko. Hata hivyo baadaye siku hizo bwana Ntawukulilyayo aliwasafirisha askari hadi mlima Kibuye ambako waliungana na wauaji wengine kuwauwa Watutsi hao. Bwana huyo ambaye alikamatwa Oktoba 2005 awali alikana makosa yote alipopanda kizimbani Juni 2008.