Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilimo cha matuta Rwanda chatajwa kama njia ya kukabiliana na njaa

Kilimo cha matuta Rwanda chatajwa kama njia ya kukabiliana na njaa

Mradi ya kilimo wa kujenga matuta mashambani katika milima ya Cyungo nchini Rwanda umelibadili eneo hilo na kuliwezesha kupata mazao mengi ya kilimo.

Akilizuru eneo hilo mkurugenmzi wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Josette Sheeran amepongeza juhudi za kulibadili eneo hilo la milima lililokabiliwa na mmomonyoko wa udongo na kuliganya kuwa la kuzalisha mazao ya kilomo kama moja ya njia ya kukabiliana na tatizo la njaa katika eneo ambalo linatajwa kuwa moja ya maeneo maskini zaidi duniani.

Takriban watu 4000 walifanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja kujenga matuta kwenye ekari 240. Sheeran amesema kuwa kwa miaka mingi wanyeji wa Cyungo wamekuwa wakitegemea shirika la WFP kwa vyakula lakini kwa wakati huu eneo hilo linazalisha chakula cha kuwatosha wenyeji wake. Wakulima hao wanahusika na kilimo cha ngano na viazi ambavyo wanauza au kutumia kama chakula.