Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wayaondoa majina 45 kwenye orodha ya vikwazo vya Taliban

UM wayaondoa majina 45 kwenye orodha ya vikwazo vya Taliban

Kamati ya umoja wa mataifa inayohusika na ukaguzi wa karibu watu 500 ambao wanastahili kuwekewa vikwazo kwa kuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi yakiwemo ya Taliban na Al-Qaeda imeyaondoa majina 45 kutoka kwa orodha hiyo.

Wale ambao majina yao yanapatikana kwenye orodha hiyo wanakabiliwa na vikwazo vikiwemo vya usafiri , na kuzuiliwa kwa mali yao vikiwemo pia vikwazo vya silaha. Kwa sasa wanachama wote wa umoja wa mataifa wanatakiwa kuweka vikwazo dhidi Osama Bin Laden , kundi la Taliban na washirika wao.

Kamati hiyo ilichukua muda wa miezi kumi na nane kuyakagua majina 448 ambayo yalikuwa kwenye orodha hiyo nh kuondoa majina 45 huku ikiyaidhinisha majina mengine 443.