Juhudi zaendelea kurejesha hali ya utulivu katika kambi ya Kalma Darfur

Juhudi zaendelea kurejesha hali ya utulivu katika kambi ya Kalma Darfur

Hali ya utulivu imeripotiwa kurejea kwenye kambi kulikoshuhudiwa ghasia katika jimbo la darfur nchini sudan baada ya kutokea kwa mapigano wiki iliyopita.

Afisa mkuu wa vikosi vya kulinda amani katika jimbo la darfur UNAMID Mohammed Yonis aliitembelea kambi ya Kalm ambapo ghasia hizo zilitokea na kujadiliana hali ya usalama na wasimamisi wa kambi hiyo.

 Naye gavana wa jimbo la Darfur Abdul Hammid Musa ameviomba vikosi vya UNAMID kuwapokonya silaha wenyeji wa kambi hiyo waliojihami. Kwa mujibu wa UNAMID wakati wa ghasia hizo waandamanaji wengi walikuwa wamejihami na mapanga huku ikisikika milio ya risasi kote kambini ambapo watu kadha waliuawa