Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Sudan imeitaka UNAMID kuwakabidhi washukiwa sita inaowahifadhi Kalma

Serikali ya Sudan imeitaka UNAMID kuwakabidhi washukiwa sita inaowahifadhi Kalma

Serikali ya Sudan imeutaka mpango wa kulinda amani kwenye jimbo la Darfur ambao ni wa vikosi vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID kuwakabidhi watu sita inaowapa hifadhi.

Sudan inasema watu hao ni washukiwa wa chanzo cha tafrani iliyozuka wiki jana katika kambi ya wakimbizi wa ndani wa Darfur ya Kalma, ambapo watu watano waliuuawa baada ya watu wenye silaha kufyatua risasi kambini hapo. Tukio hilo lilifanyika baada ya baadhi ya wakimbizi wa ndani kuhudhuria mazungumzo ya amani baina ya kundi la JLM na serikali yaliyofanyika mjini Doha Qatar.

Ndani ya kambi hiyo ya Kalma kuna wanaounga mkono mchakato wa amani na wanaopinga. Christopher Cycmanick ni msemaji wa UNAMID anafafanua kuhusu suala la watu hao.

(SAUTI YA CHRISTOPHER CYMANICK)