Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ajadili upokonyaji wa silaha na waziri wa mambo ya nje wa Japan

Ban ajadili upokonyaji wa silaha na waziri wa mambo ya nje wa Japan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye yuko ziarani nchini Japan leo amekutana na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Katsuya Okada.

Viongozi hao wawili wamejadili masula mbalimbali ikiwemo upokonyaji na kutozalisha silaha za nyuklia na pia masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa. Kesho Jumatano Ban Ki-moon atakutana na waziri mkuu Naoto Kan na kisha kuhudhuria sherehe za amani za kumbukumbu ya Hiroshima. Kama anavyosema mwakilishi wa Katibu Mkuu katika masuala ya upokonyaji silaha Sergio Duarte Ban anakuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhudhuria kumbukumbu hizo.

(SAUTI SERGIO  DUARTE )

Katibu Mkuu pia atazuru Nagasaki. Marekani iliangusha bomu la kwanza la atomic mjini Hiroshima tarehe 6 Agosti 1945 na siku tatu baadaye mjini Nagasaki. Zaidi ya watu 200,000 waliuawa kutokana na mionzi ya nyuklia na mvuke wa bomu hilo na watu wengine 400,000 wamekufa kutokana na athari za kiafya za mabomu hayo mawili ambazo zinaendelea tangu kuisha kwa vita ya pili ya dunia.