Skip to main content

UM una mikakati ya kubadili mbinu za utoaji huduma zake duniani

UM una mikakati ya kubadili mbinu za utoaji huduma zake duniani

Umoja wa Mataifa uko kwenye mikakati ya kubadili mbinu zake za kutoa huduma zake kote duniani kuhakikisha kuwa harakati hizo zinapata uungawaji mkono ili kulisadia kufanikisha huduma hizo.

Katibu mkuu wa idara inayohusika na utoaji wa huduma ya umoja wamataifa DFS Susan Malcorra amesema kuwa nchi wanachama wamependekeza njia zitakazotumika kuhakikisha huduma za umoja wa mataiafa zinatolewa kwa njia inayofaa na kwa wakati mwafaka. Kwa sasa idara ya DFS inatoa huduma za uongozi pamoja na teknolojia ya habari na mawasiliono kwa huduma 32 za vikosi vya kulinda amani vikiwemo vya muungano wa afrika nchini Somalia ,AMISON .

Mkakati huo uliafikikiwa kwenye mkutano wa umoja wa mataifa mwezi Juni mwaka huu ambapo umoja huo ulimpa idhini katibu mkuu kutenga jumla ya dola milioni 50 iwapo baraza La usalama la umoja wa mataifa litaanzisha huduma mpya au kupanua huduma zilizopo.