UM umewapongeza polisi wa Rwanda walioko Liberia kwa kazi nzuri

UM umewapongeza polisi wa Rwanda walioko Liberia kwa kazi nzuri

Naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia Hnrietta Mensa-Bonsu amewapongeza maafisa wa polisi wa Rwanda wanaofanya kazi na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo kwa utaalamu wa kazi, na nidhamu.

Amesema uwepo wao hapo umeimarisha uwezo na ujuzi wa polisi wa nchi hiyo. Akizungumza katika hafla malumu ya utowaji wa medali kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa Liberia UNMIL kutoka Rwanda jana , Bi Mensa-Bonsu amesema utekelezaji wa mfumo wa haki unasalia kuwa kiungo kikubwa cha amani na usalama nchini Liberia.

Ameongeza kuwa ingawa bado kuna changamoto, lakini changamoto hizo watazikabili taratibu, na kuesma UNMIL na washirika wake wa kitaifa na kimataifa wamejidhatiti kuliimarisha jeshi la polisi la Liberia ili kujenga imani na wananchi.