Vituo vya afya ni muhimu kuchagiza unyonyeshaji duniani:UNICEF

2 Agosti 2010

Shirika la Umoja wa Martaifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema vituo vya afya ni kmuhimu sana katika kuchagiza unyonyeshaji.

Katika wiki hii ya unyonyeshaji duniani inatakayokamilika Agosti 7, UNICEF na washirika wake wamewataka wataalamu wa afya kuwachagiza kina mama ambao wamejifungua kwa mara ya kwanza kunyonyesha watoto wao. Mkurugenzi wa UNICEF Anthony Lake amesema maziwa ya mama ni chakula bora ambacho mtoto anaweza kukipata na kunyonyesha kunatoa fursa kubwa kwa mtoto kuanza maisha.

Naye afisa wa maendeleo ya afya na watoto wachanga katika shirika la afya duniani WHO Dr Bernadette Daelmans amesema watoto milioni 1.5 kati ta milioni 8.8 wanaokufa kila mwaka maisha yao yangeweza kuonkolewa kama wangenyonya maziwa ya mama katika miezi sita ya mwanzo

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter