UNAMID inasema inajitahidi kumaliza mzozo katika kambi ya Kalma Darfur

2 Agosti 2010

Naibu mwakilishi maalumu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID kwenye jimbo la Darfur Sudan Mohamed Yonis jana amezuru Kusini mwa Darfur.

Mwakilishi huyo amekutana na gavana wa eneo hilo na viongozi wa kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kalma ambamo kulizuka machafuko baada ya baadhi ya wakimbizi wa ndani kuhudhuria mazungumzo ya amani ya Doha. Mvutano huo ulisababisha vifo vya zaidi ya watu watano.

Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa mkuu wa UNAMID Ibrahim Gambari amesema katika miezi sita ambayo amekuwa mkuu wa UNAMID hali imekuwa ikibadilika, huku miezi mine ya awali ikitoa matumaini bada ya makundi ya waasi kusaini makubaliano ya amani na serikali, lakini amesema vita baina ya makabila na mivutano baina ya wakimbizi na makundi mengine kujitoa kwenye mazungumzo vimesababisha vifo vingi. Ameongeza kuwa pia kupewa masharti na serikali ya Sudan pia kumeongeza ugumu wa UNAMID kutekeleza wajibu wake.

(SAUTI YA IBRAHIM GAMBARI)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter