Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu takribani 80 wafariki dunia kutokana na mafuriko nchini Afghanistan

Watu takribani 80 wafariki dunia kutokana na mafuriko nchini Afghanistan

watu wapatao 80 wamekufa kutokana na mafuriko makubwa yaliyoikumba eneo la mashariki mwa Afghanistan.

Misaada ya dharura inatolewa na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yakiwemo la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA na la kuhudumia watoto UNICEF na familia 4000 mashariki mwa nchi hiyo wameshaanza kupokea msaada. Hadi kufikia leo UNICEF imeshatoa mahema 430 katika majimbo ya Nangarhar na Kunar, vifaa vya kuhifadhia maji, na pia dawa za kusafisha maji zimegawiwa kwa familia 2000. Vitu vingine ni pamoja na biskuti kwa watoto 10,000 walioa chni ya miaka mitano, kina mama wajawazito na wanaonyonyesha katika mji wa Kapisa.

Kwa mujibu wa serikali ya Afghanistan maelfu ya watu wameachwa bila makao kaskazini mashariki mwa Kapisa, katikati mwa Ghazni, Laghman, Nangarhar, Kunar, Loga, Khost na Kaskazini mwa jimbo la Parwan.

Nyumba zaidi ya 4000 zimeharibiwa vibaya, huku barabara na madaraja yamebomoka. Na mwakilishi wa UNICEF nchini humo Peter Crowley amesema watoto ni muhimu wapate maji safi kuepusha magonjwa ya mlipuko.