Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pembe ya Afrika kwa mara nyingine iko huru na ugonjwa wa polio:UNICEF

Pembe ya Afrika kwa mara nyingine iko huru na ugonjwa wa polio:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na washirika wake leo wametangaza kuwa pembe ya Afrika kwa mara nyingine iko huru na virusi vya polio.

Baadhi ya nchi za pembe hiyo za Sudan, Kenya, Ethiopi na Uganda zimeelezwa kuwa kwa zaidi ya mwaka sasa hakujabaina kirusi cha polio. Shirika hilo linasema leo inaadhimisha hatua muhimu ya kuelekea kufikia mpango wa kimataifa wa kutokomeza polio Afrika.

Mkakati wa kimataifa wa kutokomeza polio unaongozwa na serikali, shirika la afya duniani WHO, bahati nasibu ya kimataifa, vituo vya kukinga na kudhibiti magonjwa Marekani CDC na UNICEF. Jumla ya watoto 101 walipooza na wengine kufariki dunia nchini Sudan, Ethiopia, Kenya na Uganda kati ya Machi 2008 na July 2009 wakati polio type 1 ilipozuka tena kwenye pembe hiyo.