Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanajeshi wa UNAMID waendesha kampeni ya usafi katika jimbo la Darfur nchini Sudan

Wanajeshi wa UNAMID waendesha kampeni ya usafi katika jimbo la Darfur nchini Sudan

Zaidi ya wanajeshi 200 wa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na kile cha muungano wa Afrika UNAMID katika jimbo la Darfur nchini Sudan hii leo wameendesha shughuli ya siku nzima ya usafi pamoja na kampeni za kuhamasisha wakaazi wa jimbo hilo kuhusisna na umihimu wa mazingira safi.

Wanajeshi hao waliendesha shughuli ya ukusanyaji wa taka na pia kuifungua mitaro ya taka na upanzi wa miti katik miji iliyo karibui na afisi za mashirika ya kimataifa. Kampeni hiyo inatarajiwa kurejelewa baada ya kila miezi miwili kama ishara ya kikosi cha UNAMID ya kutoa uhamasisho kuhusu umuhimu wa mazingira safi katika eneo hilo.