Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imesikitishwa na hatua ya kurejeshwa kwa nguvu wakimbizi wa Kisomali

UNHCR imesikitishwa na hatua ya kurejeshwa kwa nguvu wakimbizi wa Kisomali

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limesikitishwa na taarifa ya kurejeshwa nyumbani kwa nguvu wakimbizi wa Kisomali.

Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR Melissa Fleming, idadi kubwa ya wakimbizi waliokuwa Saud Arabia wamerejeshwa kwa nguvu mwezi June. Na kuongeza kuwa hali hiyo inadhihirisha bayana umuhimu wa serikali kutekeleza wito wa UNHCR wa kuyapitia upya maombi ya hifadhi ya wakimbizi kutoka maeneo ya katikati na kusini mwa Somalia.

(SAUTI YA MELISA -SOMALI)

Ameongeza kuwa UNHCR inaichukulia hatua ya kuwarejesha kwa nguvu wakimbizi na waomba hifadhi kama ni ukiukaji wa taratibu za kimataifa za kuwalinda wakimbizi na waomba hifadhi wa Kisomali hasa ikizingatiwa hali halisi ya Moghadishu.