Maziwa ya mama ni kinga, tiba na muhimu kwa maisha ya mtoto:UNICEF na WHO

30 Julai 2010

Wiki ya unyonyeshaji duniani hufanyika kila mwaka kuanzia Agosti mosi hadi 7 katika nchi zaidi ya 120.

Wiki hii hufanyika kwa lengo la kuchagiza unyonyeshaji na kuimarisha ya watoto duniani kote. Shirika la afya duniani WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wamekuwa msitari wa mbele kuchagiza kampeni za unyonyeshaji. WHO inapendekeza mtoto kunyonyeshwa hadi umri wa miezi sita na kisha kuendelea kunyonya na kula vyakula vingine hadi miaka miwili au zaidi.

Kauli mbiu ya mwaka huu wa 2010 ni "hatua 10 rafiki za unyonyeshaji wa mtoto" Hatua hizo ni kuwa na sera, kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya, kuelimisha kina mama, kuwasaidia kina mama kuanza kunyonyesha, kuwaonyesha jinsi ya kunyonyesha, kutowapa watoto wachanga chakula kingine isipokuwa maziwa ya mama, kujenga muungano baina ya mama na motto, na kuanzisha vikundi vya msaada wa kunyonyesha.

Mwaka huu jamii za Kisomali zinapewa msisitizo wa kuchagiza kina mama kunyonyesha na UNICEF imeanzisha mipango maalumu kusaidia utekelezaji, kwani wanawake wengi Somalia wananyonyesha siku tatu tuu za mwanzo baada ya mtoto kuzaliwa. Robert Kihara ni afisa mawasiliano wa UNICEF Somalia anafafanua umuhimu wa wiki ya kunyonyesha.

(SAUTI YA ROBERT KIHARA)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter