Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wapongeza kuanza utekelezaji wa mkataba wa kupinga matumizi ya mabomu mtawanyiko

UM wapongeza kuanza utekelezaji wa mkataba wa kupinga matumizi ya mabomu mtawanyiko

Mkataba wa kimataifa wa kupinga matumizi ya mambomu mtawanyiko, yaani cluster bombs, unaanza kutekelezwa Agosti mosi.

Muungano wa kupinga matumizi ya mabomu mtawanyiko ulianzishwa mwaka 2003 na wengi waliona ni ndoto kufanikisha mkataba wa kuzuia mabomu hayo. Lakini kama anavyosema Thomas Nash kutoka muungano wa kupinga mabomu mtawanyiko, miaka saba baadaye wanasherehekea kuanza kutekelezwa kwa mkataba huo.

(SAUTI YA THOMAS NASH)

Ameongeza kuwa mabomu mtawanyiko yana athari mbili kubwa kwanza yana uwezo wa kuathiri sehemu kubwa yanaporushwa, na yakitumika kwwenye eneo lenye watu wengi athari zake ni kubwa. Na pili mabomu hayo mengi hayalipuki kama yanavyotakiwa yanpogusa chini na hivyo kuzikwa kama mabomu ya kutegwa ardhini na kuendelea kusabbisha vifo au kujeruhi yanapokanyagwa.