UM umelaani walowezi wa Israel kuvamia nyumba za Wapalestina

29 Julai 2010

Mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati ,leo amelaani hatua ya walowezi wa Israel wenye silaha kuvamia kwa nguvu jengo kwenye mji wa zamani wa Jerusalem.

Mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati ,leo amelaani hatua ya walowezi wa Israel wenye silaha kuvamia kwa nguvu jengo kwenye mji wa zamani wa Jerusalem . Mji huo una una nyumba za familia tisa za Wapalestina na ametoa wito kwa serikali kuchukua hatua mara moja.

Katika taarifa yake mratibu huyo Robert Serry amesema kitendo hicho hakikubaliki na naitolea wito serikali kuwaondoa walowezi hao kutoka kwenye nyumba ya Wapalestina na kurejesha mambo kama yalivyokuwa.

Tafrani hiyo inafuatia hatua ya jana ya serikali ya Israel kubomoa majengo kadhaa ya biashara ya Wapalestina nje kidogo ya mji wa Jerusalem Mashariki.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud