Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za kumaliza mzozo wa Darfur ni changamoto kubwa:Ban

Hatua za kumaliza mzozo wa Darfur ni changamoto kubwa:Ban

Mgogoro wa Darfur unasalia kuwa moja ya changamoto kubwa zinazoikabili jumuiya ya kimataifa , miaka sita tangu suala hilo kufikishwa kwenye ajenda ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Ripoti mpya iliyotolewa leo inasema hatua za kuelekea kumaliza vita vya Darfur zimekuwa zikibadiliaka kwa miaka mingi. Inasema licha ya juhudi kubwa za mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID tangu muafaka wa amani mwaka 2006, jitihada za majadiliano ya amani zimekuwa zikikumbwa na dosari.

Kwanza ni kumeguka kwa makundi yenye silaha na pili operesheni za kijeshi zinazoendelea. Kwa mujibu wa ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kimoon mwaka 2010, kumekuwepo na dalili za kupiga hatua, lakini hatua hizo zikafuatiwa na mapigano mapya baada ya uchaguzi mwezi Mai kati ya majeshi ya serikali na kundi la Justice and Equality Movement JEM na kukiuka makubaliano waliotia sahihi mwezi Februari.